YEMENI-USALAMA

Kumi wauawa katika mapigano Yemeni

Waasi wa Kusini mwa Yemeni wakikabiliana na vikosi vya washirika wa serikali katika jimbo la Abyan, Mei 11, 2020.
Waasi wa Kusini mwa Yemeni wakikabiliana na vikosi vya washirika wa serikali katika jimbo la Abyan, Mei 11, 2020. © AFP

Mapigano yaliyozuka Kusini mwa Yemeni Jumatatu wiki hii kati ya waasi na vikosi vya washirika wa serikali vinavyojaribu kudhibiti mji wa Zinjibar, mji mkuu wa jimbo la Abyan, yamesababisha vifo vya watu kumi.

Matangazo ya kibiashara

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano hayo,kwa mujibu wa vyanzo kutoka hospitali.

Haya ni mapigano makubwa ya kwanza ya kijeshi tangu waasi wa Kusini waliotangaza jimbo lao kujitawala Aprili 26 baada ya kushindwa kwa makubaliano ya amani na serikali, makubaliano ambayo yalilikuwa yalipanga pande husika kugawana madaraka.

Kulingana na afisa wa vikosi vya waasi, vikosi vya vikosi vya tawi la kijeshi la chama cha Kiislamu cha Al-Islah - mshirika wa serikali vilizindua operesheni ya kuudhibiti mji wa Zinjibar, mji mkuu wajimbo la Abyan, huko Kusini mwa Yemen.

Waasi wamefanikiwa kukwamisha juhudi za vikosi vya serikali na washirika wake na kusababisha "vifo vingi" katika kambi ya adui na kuwakamata baadhi ya askari wao, afisa huyo, Nabil al-Hanachi, alamelihakikishia shirika la habari la AFP.

Vyanzo kutoka hospitali vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba askari wanane kutoka washirika wa serikali wameuawa na wengine 23 kujeruhiwa katika mapigano hayo.

Wapiganaji wawili kutoka kundi la waasi pia wameuawa na wengine kumi na moja kujeruhiwa, vyanzo hivyo vimesema.

Asakri na waasi waliofariki pamoja na majeruhi wamesafirishwa katika hospitali za jimbo hilo, vyanzo hivyo vimeongeza.

Tangu mwaka 2014, vita nchini Yemen kati ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na ambao wanadhibiti Kaskazini mwa nchi hiyo, na vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na muungano uanaoongozwa na Saudi Arabia tangu mwaka 2015 vimesababisha vifo vya watu wengi nchini humo.