ISRAELI-SIASA-USALAMA

Serikali mpya ya Israel kuapishwa

Benjamin Netanyahu, waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Israel, atagawana madaraka ya waziri mkuu katika msingi ya kubadilishana na hasimu wake mfuasi wa siasa za wastani Benny Gantz.
Benjamin Netanyahu, waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Israel, atagawana madaraka ya waziri mkuu katika msingi ya kubadilishana na hasimu wake mfuasi wa siasa za wastani Benny Gantz. © AFP

Baada ya siku 500 za mvutano wa kisiasa, hatimaye serikali ya umoja ya Benjamin Netanyahu na mpinzani wake wa zamani Benny Gantz inatarajiwa kuapishwa leo Alhamisi jioni na hivyo kumaliza mgogoro mrefu wa kisiasa katika historia ya Israeli.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya watu walikuwa hawajaamini na wengine bado hawajaamini kuwa serikali sasa imeundwa wakati mvutano wa kisaisa ulikuwa ukiendelea.

Benjamin Netanyahu, waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Israel ambaye anakabiliwa na kesi ya madai ya rushwa mwezi huu, atagawana madaraka ya waziri mkuu katika msingi ya kubadilishana na hasimu wake mfuasi wa siasa za wastani Benny Gantz.

Wabunge wa Israeli wanatarajia kutoa nafasi ya mwisho katika "mzozo huu wa kisiasa wa Israeli" na wakati huo huo kuanza msimu mpya wa "Serikali ya Muungano".

Hivi karibuni makundi ya upinzani yaliwasilisha mashitaka katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo yakishtumu makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita kati ya Benjamin Netanyahu na hasimu wake mkuu Benny Gantz kwa lengo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kulindoa taifa hilo la Kiyahudi kwenye mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kutokea katika nchi hiyo.

Makundi hayo yalikuwa yamebaini kwamba mashtaka ya ufisadi, udanganyifu na uvunjaji wa uaminifu yanayomkabili Bw. Netanyahu, yangemzuia kuendelea kusalia madarakani.

Mahakama Kuu ilibaini kwamba makubaliano hayo hayakiuki sheria na kwa hivyo ilikataa kuyafuta, ikiondoa kizingiti muhimu kwa muungano wa serikali.

Mashtaka ya ufisadi dhidi ya Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu hayamzuii kuunda serikali, Mahakama Kuu ya Israeli ilisema.

Hata hivyo kesi yake imepangwa kuanza Mei 24 mwaka huu.