AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Taliban yadai kutekeleza shambukizi dhidi ya jeshi la Afghanistani

Kundi la Taliban limetangaza kwamba limefanya shambulizi baya dhidi ya jeshi la Afghanistani huko Gardez, Mashariki mwa nchi hiyo, wakati, siku ya Jumanne serikali ilitangaza kuanza tena kwa mashambulizi yake dhidi ya wapiganaji wa kundi hilo.

Wanajeshi wa Afghanistan katika eneo la lashambulizi la kujitoa mhanga huko Kabul, Aprili 29, 2020.
Wanajeshi wa Afghanistan katika eneo la lashambulizi la kujitoa mhanga huko Kabul, Aprili 29, 2020. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limethibitishwa na Wizara ya Mambo ya ndani ya Afghanistani.

"Kufuatia tangazo la kuanza tena kwa mashambulizi, kuna shambulio ambalo limeendeshwa dhidi ya moja ya makao makuu muhimu ya kijeshi ya utawala wa Kabul," msemaji wa wapiganaji wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid amesema kwenye Whatsapp.

Jumatano wiki hii kundi la Taliban lilitangaza kwamba liko tayari kupigana na vikosi vya Afghanistani baada ya agizo la rais Ashraf Ghani la kuvitaka vikosi vyake kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya ya kundi hilo kufuatia shambulio baya la Jumanne lililoweka hatarini mchakato dhaifu wa amani.

"Kuanzia sasa serikali ya Kabul ndio itabebea mzigo wa lawama kwa kusababisha vurugu kuongezeka," kundi la Taliban lilibaini katika taarifa, huku likiongeza kwamba liko tayari kujibu shambulizi lolote kutoka jeshi la Afghanistani.

Hivi karibuni Mjumbe wa Marekani kwa Afghanistan, katika mazungumzo mapya Zalmay Khalilzad alilitaka kundi la Taliban kusitisha mapigano na kushikilia makubaliano ya miezi miwili yaliyotiwa saini na yanayolenga kumaliza vita nchini Afghanistan.

Chini ya makubaliano na wapiganaji hao wa Kiislamu, Marekani imeanza kuondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan kama sehemu ya mpango wa Rais Donald Trump wa kusitisha vita vya Marekani vilivyodumu kwa muda mrefu zaidi.