Hafla ya kuapishwa kwa serikali mpya Israeli yaahirishwa
Imechapishwa:
Hafla ya kuapishwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Israel iliostahili kufanyika Alhamisi wiki hii imearishwa hadi jumapili,baada viongozi watakaoendesha serikali hiyo kukosa kukubaliana kuhusu baraza la mawaziri.
Waziri mkuu Benjamin Netenyahu anatarajiwa kuongoza kwa miezi 18 kabla ya mpinzani wake mkuu Benny Gantz kuchukuwa hatamu za uongozi,kwa mjibu wa makubaliano yao.
Netanyahu na Gantz , mkuu wa zamani wa jeshi, wametangaza mwezi uliopita wataweka kando tofauti zao na uadui na kujiunga pamoja kuielekeza nchi hiyo kupitia katika mzozo wa virusi vya corona pamoja na hali mbaya ya kiuchumi.
Makubaliano hayo hata hivyo, yamesababisha kusambaratika kwa chama cha Gantz cha Bluu na Nyeupe, na kuvunja ahadi yake ya kampeni ya kutohudumu chini ya Netanyahu, anaesubiri kupandishwa kizimbani kwa mashtaka ya rushwa.