AFGHANISTANI-MAREKANI-USALAMA

Marekani yashtumu IS kuhusika na shambulio dhidi ya hospitali Kabul

Marekani imebaini kwamba kundi la wanajihadi lenye mafungamano na kundi la Islamic State (IS) ndilo liliendesha mashambulizi mawili Jumanne wiki hii nchini Afghanistan.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan kitoq ulinzi nje ya hospitali iliyolengwq na shambulio huko Kabul, Mei 12, 2020.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan kitoq ulinzi nje ya hospitali iliyolengwq na shambulio huko Kabul, Mei 12, 2020. REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Moja kati ya mashambulizi hayo mawili lilitekelezwa dhidi ya hospitali moja jijini Kabul na kuua watu 16 wakiwemo watoto wachanga wawili, amesema mjumbe maalum wa Marekani nchini Afghanistan.

Akiongea kupitia Twitter, Zalmay Khalilzad amesema kuwa raia wa Afghani hawapaswi "kuanguka katika mtego" uliowekwa na IS, lakini badala yake washikamane pamoja dhidi ya tishio hili na waweze "kupate fursa ya kutunza amani ya kihistoria" kwa taifa lao.

Waasi wa Taliban, ambao Marekani inajaribu kuhusisha katika mazungumzo ya amani na serikali ya Afghanistan, wamekanusha kuhusika kwao katika mashambulizi hayo mawili.

Kulingana na mtandao wa SITE Intel, wa shirika la Marekani ambalo linafuatilia shughuli za msimamo mkali wa makundi ya Kiislamu, tawi la IS katika ukanda huo lilidai kuhusika na shambulio hilo la kujitoa mhanga katika mkoa wa Nangarhar, Mashariki mwa nchi, ambalo ambalo liligharimu maisha ya watu 24 na wengine 68 kujeruhiwa.

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulio lililotokea katika hospitali ya Kabul, ambapo shirika la kibinadamu la Médecins Sans Frontières (MSF) linatoa huduma zake kwa wazazi wajawazito na wale wanaojifunguwa.