ISRAELI-PALSTINA-HAKI

Israel: Mlowezi wa Kiyahudi ahukumiwa kwa mauaji ya raia watatu wa Palestina

Amiram Ben-Ouliel, Mlowezi wa Kiyahudi akipelekwa na polisi katika mahakama ya Lod katikati mwa Israeli Mei 18, 2020, ambapo amehukumiwa kwa kosa la kuua watu watatu, raia wa Kipalestina, mtoto mchanga na wazazi wake wawili.
Amiram Ben-Ouliel, Mlowezi wa Kiyahudi akipelekwa na polisi katika mahakama ya Lod katikati mwa Israeli Mei 18, 2020, ambapo amehukumiwa kwa kosa la kuua watu watatu, raia wa Kipalestina, mtoto mchanga na wazazi wake wawili. AFP

Mlowezi mmoja wa Kiyahudi aliyepatikana na hatia ya mauaji ya mtoto mchanga na wazazi wake, raia wa Palestina waliouawa baada ya nyumba yao kushambuliwa kwa moto mwaka 2015 katika Ukindo wa Magharibi.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Lod, katikati mwa Israel, pia imempata Amiram Ben-Ouliel na hatia ya kujaribu kuua, kuteketeza kwa moto nuymba ya wahanga na uhalifu wa kibaguzi.

Mezi Julai 2015, mtoto wa miezi 18, Ali Dawabcheh, alichomwa moto akiwa amelala, baada ya vifaa vya moto kurushwa dhidi ya nyumba yao huko Douma, kati ya Nablus na Ramallah katika Ukingo wa Magharibi, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli tangu mwaka 1967.

Baba yake Saad na mama yake Liham, walipoteza maisha wili zilizofuata kutokana na maeraha walioyapata wakiwa usingizini kufuatia shambulizi hilo la moto. Ndugu wa mtoto mtoto mchanga aliyefariki, Ahmed tu, wakati ho akiwa na umri wa miaka minne, ndiye aliyenusurika katika janga hilo.

Hukumu ya Amiram Ben-Ouliel, ambaye alikuwa mtuhumiwa mkuu katika kesi hii, haijulikani.

Shirika la Honenou kutoka Israel, ambalo lilisaidia kwa upande wa utetezi wa mshtumiwa, limesema litakataa rufaa mbele ya Mahakama Kuu.

Amiram Ben-Ouliel alikataa kutoa ushahidi wakati wa kesi yake na amehukumiwa kwa msingi wa kukiri kwake wakati wa alipokuwa akihojiwa katika ofisi ya mwendesha mashitaka.

Wakili wake, Asher Ahayon, kwenye Redio ya Kan leo Jumatatu alikosoa namna mteja wake alivyokiri makosa yake akisema kuwa alifanya hivyo baada ya"kupata mateso kwa wiki tatu" kutoka kitengo cha cha polisi ya Israeli cha Shin Bet.

"Bado hatujatendewa haki kwa sababu tuna uhakika kuwa moto huo shambulio hilo halikutekelezwa na mtu mmoja," amesikitika Nasser Dawabcheh, mjomba wa mtoto, baada ya hukumu kutangazwa.

Mauaji hayo watu watatu yalizua hisia tofauti katika maeneo ya Palestina lakini pia nje ya nchi na nchini Israel.