SYRIA-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Syria: Pande hasimu zakubali kuendelea na mazungumzo Geneva

Geir Pedersen hakutangaza tarehe ya kuanza kwa mazungumzo hayo na amesema kwamba mkutano huo wa Kamati ya Katiba ya Syria - inayoundwa na wawakilishi wa serikali ya Bashar al Assad, upinzani na mashirika ya kiraia - hautafanyika kupitia video.
Geir Pedersen hakutangaza tarehe ya kuanza kwa mazungumzo hayo na amesema kwamba mkutano huo wa Kamati ya Katiba ya Syria - inayoundwa na wawakilishi wa serikali ya Bashar al Assad, upinzani na mashirika ya kiraia - hautafanyika kupitia video. REUTERS

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria ametangaza kwamba pande hasimu katika mgogoro unaoendelea nchini humo zimekubaliana kukutana tena kwa mazungumzo huko Geneva.

Matangazo ya kibiashara

Pande mbalimbali zinazohusika katika mgogoro unaoendelea nchini Syria zimekubali kukutana kwa mara nyingine kwa mazungumzo mara tu hali ya afya itakaporuhusu, ili kuendelea na mazungumzo kuhusu katiba, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Geir Pedersen, amesema.

"Mara tu hali ya janga (ya Covid-19) itaruhusu, wamekubaliana kwenda Geneva na wakakubaliana kuhusu ajenda ya mkutano ujao," Geir Pedersen ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari.

Geir Pedersen hakutangaza tarehe ya kuanza kwa mazungumzo hayo na amesema kuwa mkutano huo wa Kamati ya Katiba ya Syria - inayoundwa na wawakilishi wa serikali ya Bashar al Assad, upinzani na mashirika ya kiraia - hautafanyika kupitia video.

Kamati ya Katiba ya Syria ilikutana kwa mara ya kwanza katika majira ya Joto nchini Geneva chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa.