PAKISTAN_AJALi-USALAMA

Ajali ya ndege ya watu zaidi ya 11 Pakistani

Ndege ya Shirika la kimataifa la ndege la Pakistani, Pakistan International, imeanguka katika makazi ya watu ya Model Colony huko Karachi, nchini Pakistani, vyanzo vya usalama vimebaini.

Gari ya wagonjwa ikiwasili kwenye eneo la ajali katika eneo la makazi la Karachi, Pakistan, Mei 22, 2020.
Gari ya wagonjwa ikiwasili kwenye eneo la ajali katika eneo la makazi la Karachi, Pakistan, Mei 22, 2020. REUTERS/Akhtar Soomro
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya usimamizi wa safari za ndege nchini Pakistan, imesema kuwa, ndege hiyo iliyoanguka wakati ikitua na kulipuka huku makaazi ya watu yakiteketea kwa moto.

Msemaji wa Mamlaka hayo Abdullah Hafeez amesema kuwa abiria 91 na wafanyikazi saba ndio waliokuwa ndani ya ndege hiyo iliyopoteza mwelekeo.

Hadi sasa, mamlaka ya safari za ndege nchini humo inasema, uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo lakini maneno ya mwisho ya rubani huyo, alisikika akisema kuna hitilafu ya kimitambo

Kabla ya kuanguka, ndege hiyo ilikuwa imeondoka mjini Lahore, ikielekea katika mji wa Karachi, mji mkubwa nchini humo.