IRAN-CORONA-AFYA

Iraq: coronavirus, mgogoro unaosababisha migogoro kadhaa

Mmoja wa waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga serikali kwenye Daraja la Al-Jumhuriyah huko Baghdad, Iraq, Mei 10, 2020.
Mmoja wa waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga serikali kwenye Daraja la Al-Jumhuriyah huko Baghdad, Iraq, Mei 10, 2020. AHMAD AL-RUBAYE / AFP

Nchini Iraq, idadi ya kesi za Covid-19 bado ni mdogo kama ilivyo katika nchi nyingi za Mashariki ya Kati. Lakini athari za kiuchumi kutokana na mgogoro huu wa kiafya tayari zinaonekana kuwa mbaya katika nchi hii ambayo inaelekea pabaya.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Iraq imerekodi kesi 3,877 za maambukizi ya Covid-19 baada ya visa vipya 153 kuthibitishwa na vifo 140, kulingana na takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Wagonjwa 2,483 wamepona kulingana na chanzo hicho.

Hata kama Umoja wa Mataifa unabaini kwamba takwimu hizi zinaweza kuwa juu zaidi, hasa kutokana na idadi ndogo ya vipimo katika nchi hii yenye wakazi Milioni 40, "viongozi wamedhibiti mgogoro huo vizuri," amesema Caroline Séguin, mkuu wa shirika la Madaktari wasio na Mipaka Mashariki ya Kati.

Hatua zilichukuliwa haraka sana lakini hali mbaya bado inaweza kutokea baadae, "kutokana na kupuuzia kwa hatua hizi na changamoto mbali mbali ambazo serikali mpya inatarajia kukabiliana nazo; ikiwa ni pamoja na mgogoro mkubwa wa kiuchumi na kutokea kwa machafuko mapya nchini humo".

Wakati huo huo katika nchi jirani ya Iran mambo sio mazuri na hali inaendelea kutisha.

Iran kwa sasa inakabiliwa na mripuko mbaya zaidi wa maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo la Mashariki ya Kati, huku wasiwasi pia ukizidi katika Ukanda wa Gaza na Yemen kutokana na ongezeko la idadi ya maambukizi hayo.

Virusi vya corona vimewaathiri wahudumu wa afya wapatao 10,000 nchini Iran, kulingana na taarifa za vyombo vya habari za jana Alhamisi zilizomnukuu Naibu Waziri wa Afya Qassem Janbabaei, ambaye hakufafanua zaidi.