SAUDI -ARABIA-USALAMA-MAUAJI

Sita wauawa kwa kupigwa risasi Kusini mwa Saudi Arabia

Saudi Arabia inaoongoza muungano wa nchi za Ghuba zilizoingilia kijeshi nchini Yemen dhidi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Waashia kutoka Iran, ambao wamedhibiti miji mikubwa ya nchi hiyo tangu mwishoni mwa mwaka wa 2014.
Saudi Arabia inaoongoza muungano wa nchi za Ghuba zilizoingilia kijeshi nchini Yemen dhidi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Waashia kutoka Iran, ambao wamedhibiti miji mikubwa ya nchi hiyo tangu mwishoni mwa mwaka wa 2014. RFI

Shirika la habari la SPA limeripoti kwamba watu sita wameuawa kwa kupigwa risasi Kusini mwa Saudi Arabia, taarifa ambayo inathibitishwa na vyanzo kadhaa vya serikali.

Matangazo ya kibiashara

Polisi ya Saudia imeanzisha uchunguzi baada ya tukio hilo la mauaji ya watu lililotokea karibu na jimbo la Asir, mkoa unaopatikana.

Katika tukio hilo, raia watatu kutoka Saudi Arabia pia wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali, shirika la habari la SPA limesema.

Hata hivyo shirika hilo la PSA halikutoa maelezo yoyote juu ya tukio hilo lililotokea huko Al Amwah, Kusini mwa Saudi Arabia.