SYRIA-UTURUKI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Ankara yayashushia lawama makundi yenye silaha kuvuruga usalama Idlib

Le président turc Recep Tayyip Erdogan lors de sa rencontre avec le vice-président américain Mike Pence, jeudi.
Le président turc Recep Tayyip Erdogan lors de sa rencontre avec le vice-président américain Mike Pence, jeudi. REUTERS/Huseyin Aldemir

Makundi yenye itikadi kali yanajaribu kuvuruga mkataba wa usitishwaji mapigano katika mkoa wa Siria wa Idlib, uliofikiwa mwanzoni mwa mwezi Machi kati ya Moscow na Ankara, lakini mkataba huo bado upo, Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amesema.

Matangazo ya kibiashara

"Makundi yenye itikadi kali, makundi yasiyojulikana yanayoendelea na malengo yao wenyewe, yamejaribu kuvuruga mkataba wa usitishwaji mapigano, lakini kwa sasa tuko kwenye mazungumzo na wenzetu wa Urusi na makubaliano yaliyofikiwa Machi 5 bado yanatekelezwa", Hulusi Akar ameiambia runinga ya kitaifa ya A Haber.

Mapema wiki hii rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alishtumu serikali ya Syria kwamba imeongeza uchochezi katika mkoa huo wa Kaskazini-magharibi mwa Syria, ambapo ndege za kivita za Urusi, kulingana na mashuhuda, zilitekeleza mashambulizi katika vijiji vinavyoshikiliwa na makundi ya waasi Jumatatu wiki hii.

Uturuki hautaruhusu mkoa wa Idlib kuwa eneo la migogoro tena, rais Recep Tayyip Erdogan amebaini.

Waziri wake wa Ulinzi hakutaja mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa Jumatatu wiki hii, ambayo ni mashambulizi ya kwanza katika mkoa huo tangu kutiliwa saini mkataba wa usitishwaji mapigano kati ya Urusi na Uturuki.

Huko Moscow, shirika la habari la Tass liliripoti Jumatano wiki hii kwamba Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan wamezungumzia swall la Idlib wakati wa mazungumzo yao kwa njia ya simu.