UN-UMOJA WA KIARABU-ISRAEL-PALESTINA-AMANI-USALAMA

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Kiarabu waitaka Israel kusitisha mpango wake kwa maeneo ya Palestina

Kiongozi wa nchi za Umoja wa Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, amesema hatua ya Israeli ya kuchukua maeneo ya Ukingo wa Magharibi itarudisha nyuma harakati za Palestina kuwa taifa huru.
Kiongozi wa nchi za Umoja wa Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, amesema hatua ya Israeli ya kuchukua maeneo ya Ukingo wa Magharibi itarudisha nyuma harakati za Palestina kuwa taifa huru. murad FATHI / Arab League / AFP

Umoja wa Mataifa na umoja wa nchi za kiarabu, zinaonya kuwa iwapo Israeli itaendelea na mpango wake wa kuchukua maeneo ya Ukingo wa Magharibi, unaokaliwa na Wapalestina, kitendo hicho kitakuwa ni kinyume cha sheria za Kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa nchi za Umoja wa Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, amesema hatua hiyo itarudisha nyuma harakati za Palestina kuwa taifa huru.

Kwa upande mwingingne Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ameonya kuwa hatua ya Israel ya kuchukua maeneo ya Ukingo wa Magharibi, itarudisha nyuma jitihada za kupata amani ya kudumu kati ya Israel na Palestina.

"Kama mpango huo, utatekelezwa, inaweza kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa, na hivyo itahatarisha juhudi za kupata suluhisho kati ya nchi hizo mbili na itapunguza uwezekano wa kuanza tena kwa mazungumzo," Antonio Guterres amesema mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

"Ninatoa wito kwa serikali ya Israeli kuachana na mipango yake ya kudhibiti eneo la Ukanda wa Magharibi," ameongeza.

Guterres amesema katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press (AP) kuwa Umoja wa mataifa umekuwa ukitoa mara kwa mara ujumbe kuwa unyakuaji huo hautakuwa tu dhidi ya sheria za kimataifa lakini utakuwa tukio kubwa la kuyumbisha usalama wa Mashariki ya Kati.

Mpango huu wa Israel unaungwa mkono na Marekani.