ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-USALAMA

Israeli yafanya mashambulizi ya anga Gaza

Katika muendelezo huo wa uhasama kati ya Israeli na Palestina, vikosi vya Israeli vimeshambulia 'viwanda' vya kutengeneza vifa vya jeshi na roketi Kusini mwa Ukanda wa Gaza, jeshi la Israeli limesema.
Katika muendelezo huo wa uhasama kati ya Israeli na Palestina, vikosi vya Israeli vimeshambulia 'viwanda' vya kutengeneza vifa vya jeshi na roketi Kusini mwa Ukanda wa Gaza, jeshi la Israeli limesema. REUTERS/Amir Cohen

Jeshi la wanaanga la Israeli limeetekeleza mashambulizi dhidi ya ngome za wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza usiku wa Ijumaa kuamkia leo Jumamosi baada ya wanamgambo wa kundi hilo kurusha roketi nchini Israeli.

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo yanatokea katika hali ya mvutano mkubwa ikikaribia muda wa mwisho kuhusu mpango wa Israel wa kunyakuwa maeneo ya Ukingo wa Magharibi.

Ijumaa jioni makombora mawili yalirushwa kutoka Gaza kuelekea Israeli bila kusababisha hasara yoyote. Idara ya huduma za dharura imebaini kwamba kengele za tahadhari zilisikika huko Sderot, mji wa Israeli unaopatikana kilomita chache na Palestina.

Katika muendelezo huo wa uhasama kati ya Israeli na Palestina, vikosi vya Israeli vimeshambulia 'viwanda' vya kutengeneza vifa vya jeshi na roketi Kusini mwa Ukanda wa Gaza, jeshi la Israeli limesema leo Jumamosi.

Vyanzo vya usalama huko Gaza vimelithibitisha shirika la habari la AFP kuhusu mashambulizi hayo katika eneo la Khan Younes, katika ncha ya Kusini mwa Palestina lenye wakazi milioni mbili.

Siku ya alhamisi tawi la kijeshi la Hamas lilionya Israeli kuhusu mpango wake wa kunyakuwa maeneo ya Ukingo wa Magharibi, ikilinganisha mpango huo na tangazo la vita.