ISRAELI-SYRIA-USALAMA

Israeli: Tumelipiza kisasi dhidi ya ngome za jeshi la Syria

Hezbollah, kundi la wanamgambo wa Kishia  wenye silaha, imewapeleka wapiganaji kwenda Syria kama sehemu ya msaada wa Tehran kwa serikali ya Bashar al-Assad tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2011.
Hezbollah, kundi la wanamgambo wa Kishia wenye silaha, imewapeleka wapiganaji kwenda Syria kama sehemu ya msaada wa Tehran kwa serikali ya Bashar al-Assad tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2011. JALAA MAREY / AFP

Majeshi ya Israeli yamesema na kujigamba kuwa helikopta zake zilifanya mashambulizi dhidi ya ngome za jeshi la Syria ikiwa ni jibu la kulipiza kisasi kwa shambulizi la maroketi yaliyorushwa dhidi ya eneo la milimani la Golan, linalo kaliwa na taifa hilo la Kiyahudi.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, jeshi la Israeli limebaini kwamba limelenga hasa vituo vya uchunguzi na mifumo ya ukusanyaji wa taarifa za kijasusi vinavyopatikana katika kambi ya vikosi vya jeshi la Syria.

Shambulio hilo la angani linakuja saa kadhaa baada yajeshi la Israeli kuripoti kwamba milipuko kadhaa ilisikika kutoka eneo la Golan linalodhibitiwa na Syria. Hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Shirika la habari la serikali ya Syria, likinukuu chanzo kutoka jeshi, limebaini kwamba ngome tatu za jeshi zinazopatikana karibu na mji wa Qouneitra, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo ziliharibiwa na makombora yaliyorushwa, na kuwajeruhi watu wawili na kusababisha hasara kubwa.

Mivutano kando na mpaka wa Syria na Israeli umeongezeka wiki hii baada ya mpiganaji wa Hezbollah anayeungwa mkono wa Iran kuuawa katika shambulizi la anga la Israeli katika mji wa Damascus Jumatatu wiki hii.

Hezbollah, kundi la wanamgambo wa Kishia wenye silaha, imewapeleka wapiganaji kwenda Syria kama sehemu ya msaada wa Tehran kwa serikali ya Bashar al-Assad tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2011.

Israel inaona uwepo wa Irani na Hezbollah nchini Syria kama tishio la kimkakati na imefanya mamia ya mashambulizi ya anga dhidi ya mali zinazodai kuwa za Iran.