ISRAELI-NETANYAHU-SIASA

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aingia vitani na vyombo vya habari

Benjamin Netanyahu, Juni 14, 2020.
Benjamin Netanyahu, Juni 14, 2020. Sebastian Scheiner/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Israeli Benyamin Netanyahu ameshutumu vyombo vya habari vyenye kuegemea upande mmoja kupotosha ukweli na kuchochea maandamano ili kutaka ajiuzulu. Benjamin Netanyahu amevifananisha vyombo hivyo ka vile vya Korea Kaskazi.

Matangazo ya kibiashara

Netanyahu pia ameshutumu vyombo vya habari kwa "kupuuzia machafuko yanayosabbishwa na waandamanaji na wito unaotolewa wa kumuua waziri mkuu na familia yake."

Akiongea kwa ghadhabu wakati wa mkutano wa baraza lake la mawaziri, Netanyahu amevikosoa vyombo vya habari kwa kuchochea maandamano hayo na kwa kupotosha ukweli wa matukio ya vurugu dhidi ya waandamanaji.

Kwa karibu miezi miwili, maandamano yameongezeka, hasa mbele ya makazi ya Waziri Mkuu huko Jerusalemu, na kwa mara kadhaa yamegeuka na kuwa ya vurugu.

Waziri Mkuu wa Israel amelaani vurugu kutoka pande zote lakini wakati huo huo ameashutumu waandamanaji wanaomtaka ajiuzulu "kuvunja demokrasia" na kuunda kuunda kundi halisi ili kueneza virusi vya Corona. Huu ni mzozo mpya ndani ya serikali wakati vyama vikuu viwili vinavyounda serikali hiyo, Likud na Blue and White, hawajafikia makubaliano juu ya sheria ya bajeti, hali ambayo inaweza kusababisha moja kwa moja uchaguzi mpya.