LEBANON-UFARANSA-UCHUNGUZI-USALAMA

Emmanuel Macron atoa wito kwa viongozi wa Lebanon kufanya mageuzi ya haraka

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizuru mitaa ya Beirut iliyoharibiwa Agosti 6, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizuru mitaa ya Beirut iliyoharibiwa Agosti 6, 2020. THIBAULT CAMUS / POOL / AFP

Ufaransa itaendelea kuisaidia Lebanon baada ya janga la Jumanne, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi leo Alhamisi, baada ya kuzuru Beirut, huku akiomba kutekelezwa kwa haraka mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

"Nimekuja hapa kuzungumza na kutoa msaada uliotolewa na taifa la Ufaransa, raia wa Ufaransa, kwa raia wa Lebanon," amesema rais wa Ufaransa.

Ametaka uchunguzi wa mlipuko wa Jumanne katika bandari ya Beirut "ufanyike haraka iwezekanavyo ndani ya mfumo huru na wa wazi ili kuelezea na kutoa ripoti ya kile kilichotokea".

Rais Macron amesisitiza haja ya kuwepo na "mipango madhubuti (...) ili kupambana dhidi ya rushwa, kuweka uwazi katika mambo mbalimbali, kutekeleza marekebisho ambayo tunayajua", akitoa mfano wa mapambano dhidi ya rushwa, mageuzi ya mfumo wa benki na mageuzi ya sekta ya umeme.

"Ni kwa viongozi leo, kwa raia walio huru, kutekeleza maamuzi haya," ameongeza Emmanuel Macron kabla ya kukutana na viongozi wa kisiasa wa Lebanon.