LEBANON-UFARANSA-UCHUNGUZI-USALAMA

Emmanuel Macron atoa wito kwa viongozi wa Lebanon 'kufanya mabadiliko makubwa'

Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari huko Beirut, Agosti 6, 2020.
Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari huko Beirut, Agosti 6, 2020. AP Photo/Thibault Camus, Pool

Waandamanaji wenye hasira wamekabiliana na maafisa wa usalama jijini Beirut nchini Lebanon wakilaani mlipuko uliotokea katika ghala la kuhifadhi kemikali wiki hii na kusababisha vifo vya zaidia ya watu 140 na kuwajeruhi wengine zaidi ya Elfu Tano.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wanailaumu serikali kwa  utepetevu, suala ambalo wanaamini lilicha lilisabababisha mlipuko huo mkubwa na sasa wanataka uchunguzi wa Kimataifa kufanyika.

Wakati maandamano hayo yakifanyika, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa ziarani nchini humo kwenda kujionea uharibufu uliotokea na kutoa wito wa kufanyika mabadiliko ya haraka ya kisiasa nchini humo.

Umati uliojitokeza kumkaribisha Macron ulipiga kelele na kutamka maneno ya kuwapinga viongozi wa kisiasa na ufisadi uliokithiri.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewaahidi Walebanon kuwa msaada wa kuujenga upya mji huo hautakwenda katika mikono ya mafisadi na akawahimiza maafisa wa kisiasa kufanya mageuzi au waitumbukize Lebanon katika mgogoro mkubwa.