LEBANON-UCHUNGUZI-USALAMA

Maafisa 16 wa bandari ya Beirut wakamatwa

Mlipuko mkubwa uliotokea kwene bandari ya Beirut uligharimu maisha ya watu zaidi ya 137 na 5,000 kujeruhiwa.
Mlipuko mkubwa uliotokea kwene bandari ya Beirut uligharimu maisha ya watu zaidi ya 137 na 5,000 kujeruhiwa. Thibault Camus/Pool via REUTERS

Watu kadhaa wamekamatwa huko Beirut, nchini Lebanon baada ya mlipuko mkubwa uliogharimu maisha ya watu zaidi ya 137 na 5,000 kujeruhiwa. Watu hao wote ni wafanyakazi wa bandari ya mji mkuu wa Lebanon. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Matangazo ya kibiashara

Wachunguzi wanatathmini iwapo utunzaji wa kemikali aina ya ammonium nitrate, inayoaminika kusababisha milipuko hiyo mikubwa, ilifanyika kwa makusudi.

Maafisa 16 kutoka bandari ya Beirut na viongozi wa forodha wametiwa nguvuni, bila kujua tarehe halisi ya kukamatwa kwao, ameripoti mwandishi wetu Pierre Olivier.

Hatua ya kukamatwa kwa watu hao ni ishara kubwa kwa raia wa Lebanon ambao wanasubiri haki itendekea na wahusika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Rais wa Ufaransa ambaye yuko ziarani nchini Lebanon ametaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike kubaini ukweli kuhusu mlipuko huyo, huku akitoa wito kwa viongozi wa Lebanon 'kufanya mabadiliko makubwa' ya kisiasa.