LEBANON-MSAADA-UCHUMI

Lebanon: Jamii ya kimataifa yakubaliana kuhusu msaada wa zaidi ya Euro milioni 250

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa mkutano wa kimataifa kwa njia ya video kuhusu Lebanon, Agosti 9, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa mkutano wa kimataifa kwa njia ya video kuhusu Lebanon, Agosti 9, 2020. Christophe Simon/Reuters

Wakati wa mkutano kwa njia ya video uliofanyika Jumapili, Agosti 9, nchi zilizoamua kusaidia Lebanon baada ya mlipuko ambao uliuthiri mji wa Beirut, zimekubaliana kwamba msaada wa zaidi ya Euro milioni 250 utasimamiwa na Umoja wa Mataifa na kutolewa kwa uwazi kamili kwa wananchi wa Lebanon.

Matangazo ya kibiashara

Karibu wawakilishi thelathini wa nchi zilizojitolea kusaidia Lebanon walikutana Jumapili alasiri, Agosti 9 kupitia video, mkutano ambao uliandaliwa kwa ushirikiano na Ufaransa na Umoja wa Mataifa (UN).

Lengo ilikuwa kuchangisha fedha na msaada mwingine wa kupunguza athari za janga lililoikumba Lebanon, inayokabiliwa na mdororo wa kiuchumi.

Lebanon ilikumbwa na mlipuko mbaya uliotokea Jumanne huko Beirut ambao uligharimu maisha ya watu 158 na 6,000 kujeruhiwa.

Wakati huo huo rais wa Ufaransa Emanuel Macron leo ameitaka jumuiya ya kimataifa kuharakisha msaada wa kiutu kwa Lebanon na kuwatolea wito viongozi wa taifa hilo kuzuia machafuko baada ya mlipuko mkubwa kusababisha maafa mjini Beirut.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na rais Doland Trump wa Marekani, Michel Aoun wa Lebanon na wawakilishi wa serikali kadhaa na mashirika ya kimataifa, Macron amesema ulimwengu unapaswa kuisadia Lebanon haraka iwezekanavyo na kuepusha taifa hilo kutumbukia kwenye machafuko. Macron alikua kiongozi wa kwanza wa kigeni kuitembelea Lebanon baada ya mlipuko wa siku ya Jumanne.