LEBANON-USALAMA

Lebanon: Ufaransa yataka 'kuundwa haraka kwa serikali inayozingatia majukumu yake'

Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab, kwenye makao makuu ya serikali huko Beirut, Agosti 10, 2020
Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab, kwenye makao makuu ya serikali huko Beirut, Agosti 10, 2020 Mohamed Akazir/Reuters

Ufaransa imezungumzia kuhusu kujiuzulu kwa serikali ya Lebanon, uamuzi uliyochukuliwa Jumatatu Agosti 10 na Waziri Mkuu wa Lebanoni Hassan Diab.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, amebaini kwamba, "kitu muhimu zaii kwa nchi ya Lebanon ni kuundwa haraka kwa serikali ambayo inazingatia majukumu yake kwa wananchi wa Lebanon na ambayo itakuwa na majukumu wa kujibu changamoto kuu zinazoibali nchi hiyo, hususan ujenzi wa mji wa Beirut na mageuzi katika sekta mbalimbali, ikilinganishwa na jinsi nchi hiyo inaelekea katika mdororo wa kiuchumi, kijamii na kisiasa ”.

Serikali ya Hassan Diab ilijiuzulu chini ya shinikizo kutoka kwa raia wa nchi hiyo walioghadhabishwa na matatizo mbalimbali pamoja na mlipuko mbaya uliotokea katika bandari ya mji mkuu wa nchi hiyo Agosti 4.

Mlipuko hu uligharimu maisha ya watu angalau 160 na zaidi ya 6,000 kujeruhiwa, pamoja na uharibifu mkubwa sana.

Hata hivyo Waziri mkuu wa Lebanon Hassan Diab ametangaza kujiuzulu kwa serikali kufuatia mripuko wa wiki iliyopita mjini Beirut na kusababisha madhara makubwa kuanzia makazi ya watu, vifo na hata majeruhi.

Waziri Mkuu wa Lebaoni Hassan Diab amesema "ufisadi ndio chanzo cha janga hili.”

Baadhi ya mawaziri tayari walikuwa wamejiuzulu hapo kabla, kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali yaliyoibuka baada ya mripuko huo kutokea.