AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: Watu wengi wajeruhiwa katika milipuko ya roketi Kabul

Wafanyakazi wote kutoka balozi mbalimbali katika eneo hilo wamepelekwa kwenye eneo usalama, kulingana na afisa mwandamizi kutoka nchi ya Magharibi.
Wafanyakazi wote kutoka balozi mbalimbali katika eneo hilo wamepelekwa kwenye eneo usalama, kulingana na afisa mwandamizi kutoka nchi ya Magharibi. REUTERS

Mamlaka nchini Afghanistan na vyanzo vilivyo karibu na idara za usalama nchini humo wamebaini kwamba watu zaidi ya kumi, ikiwa ni pamoja na watoto wanne, wamejeruhiwa katika shambulio la roketi katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut.

Matangazo ya kibiashara

Haijulikani waliohusika wa mauaji hayo, yaliyotokea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru, lakini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ametangaza kwamba watu wawili wamekamatwa kwa uchunguzi.

Makombora manne yalirushwa karibu na 'eneo', kunakopatikana balozi kadhaa za mataifa ya kigeni na makao makuu ya vikosi vya NATO nchini Afghanistan, mashahdi wamebaini. Wafanyakazi wote kutoka balozi mbalimbali katika eneo hilo wamepelekwa kwenye eneo usalama, kulingana na afisa mwandamizi kutoka nchi ya Magharibi.

Kundi la Taliban lilifikia mkataba na Marekani mwezi Februari, mkataba ambao unaitaka Marekani kuondoa askari wake nchini Afghanistan katika kipindi cha miezi 14 na kuazishwa kwa mazungumzo na serikali ya Afghanistan, lakini mapigano bado yanaendelea kurindima nchini humo.

Wakati huo huo Afghanistan imesitisha zoezi la kuwaachia wafungwa wa Taliban ikitaka kundi hilo pia kuwaachia maafisa wa serikali.

Mkataba wa amani baina ya Marekani na Taliban ulilitaka kundi hilo kuwaachia maafisa 1,000 wa serikali na jeshi huku serikali ikiwawachia jumla ya wafungwa 5,000 iliyokuwa ikiwashikilia.

Kwa upande wake, msemaji wa Taliban Suhail Shaheen amesema kundi hilo limetimiza wajibu wake, na hawana taarifa ya afisa yeyote wa serikali ambaye bado anashikiliwa. Kundi hilo lilisema liko tayari kuanza mazungumzo na serikali ndani ya wiki moja mara baada ya zoezi la kuwaachia wafungwa litakapokamilika.