LEBANON-HARIRI-HAKI

Kesi ya mauaji ya Rafik Hariri: Mtuhumiwa mmoja apatikana na hatia, wengine watatu wafutiwa mashitaka

Uamuzi wa mahakama ya STL ya Hague imetamatisha kesi kuhusiana na mauaji ya Rafik Hariri, iliyodumu miaka sita.
Uamuzi wa mahakama ya STL ya Hague imetamatisha kesi kuhusiana na mauaji ya Rafik Hariri, iliyodumu miaka sita. iroschka VAN DE WOUW / ANP / AFP

Mahakama Maalum ya Lebanon (STL) imempata na hatia Salim Ayyash, mwanaharakati wa Hezbollah, kuhusiana na mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri mwaka 2005. Washukiwa wengine watatu wamefutiwa mashitaka.

Matangazo ya kibiashara

"Mahakama ya mwanzo imemkuta na hatia Bwana Ayyash zaidi ya ya mauaji ya kukusudia ya Rafik Hariri," Jaji Kiongozi David Re amesema wakati Mahakama Maalum ya Lebanon (STL) ikitangaza uamuzi wake na kumaliza kesi hiyo iliyudumu miaka sita.

Washukiwa wengine watatu wamefutiwa mashitaka. "Mahakama ya mwanzo inatangaza kwamba Hassan Merhi, Hussein Oneissi na Assad Sabra hawana hatia ya mashtaka yote yaliyowasilishwa," amebaini Jaji David Re.

Hakuna hata mmoja wa washtakiwa wanne aliyekamatwa, na wote hawakuwepo mahakamani. Mtu wa tano, anayechukuliwa kama 'mhusika mkuu' wa ukatili huo, aliuawa nchini Syria mwaka 2016.

Hakuna ushahidi wa kuhusika kwa Hezbollah au Syria katika mauaji hayo.

Awali ilidaiwa kuwa Hezbollah na serikali ya Syria walihusika katika mauaji ya waziri mkuu wa zamanani wa Lebanon Rafik Hariri.

Zaidi ya watu 220 walijeruhiwa pale gari lililokuwa limejazwa vilipuzi lilipolipuka wakati msafara wa Bwana Hariri ulipokuwa unapita mbele ya ufuo wa Beirut.

Kulingana na majaji, "hakuna ushahidi kwamba uongozi wa Hezbollah ulihusika katika mauaji ya Rafik Hariri," ameripoti mwandishi wetu hukoHague, Stéphanie Maupas. Pia hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa "kuhusika kwa Syria" katika mauaji hayo. Majaji wamebaini kwamba wachunguzi na mwendesha mashtaka wameshindwa kuwatambua wadhamini wa shambulio dhidi ya Rafik Hariri.