LEBANON-HARIRI-HAKI

Mahakama Maalum ya Lebanon kutoa uamuzi kuhusu mauaji ya Hariri

Picha ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri.
Picha ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri. Reuters/ Jamal Saidi

Mahakama Maalum ya Lebanon inatarajia kutoka uamuzi wake kuhusu mauaji ya Rafik Hariri huko Hague, nchini Uholanzi, miaka kumi na tano baada ya kuuawa kwa Waziri huyo Mkuu wa zamani wa Lebanon na wengine 21 katika shambulio la bomu lililotegwa katika gari jijini Beirut.

Matangazo ya kibiashara

Asubuhi ya 14 Februari 2005, Rafik Hariri, wakati huo mbunge ambaye alijihusisha na upinzani bungeni, alikuwa kwenye msafara wake uliokuwa unapita hoteli ya St. George mjini Beirut na bomu lililokuwa limefichwa ndani ya gari likalipuka.

Hakuna hata mmoja wa washtakiwa wanne waliokamatwa. Watuhumiwa walihukumiwa na Mahakama Maalum nchini Uholanzi licha ya kutokuwepo mahakamani. Mtu wa tano, anayechukuliwa kama 'kiongozi mkuu ' wa kundi hilo, aliuawa nchini Syria mwaka 2016.

Watu zaidi ya 220 walijeruhiwa katika shambulio hilo lililolenga msafara wa Bwana Hariri ulipokuwa unapita mbele ya ufuo wa Beirut.

Kundi la Kishia la Hezbollah na Syria walihuishwa na mauaji hayo lakini wameendelea kukanusha madaia hayo.

Hadi kufikia sasa hakuna taarifa zozote kuhusu walipo washukiwa hao Salim Jamil Ayyash, Hassan Habib Merhi, Hussein Hassan Oneissi na Assad Hassan Sabra.

Wafuasi wa kundi la Hezbollah wametupilia mbali kesi hiyo wakisema kwamba mchakato wa mahakama maalum hauzingatii haki.