AFGHANISTANI-MAFURIKO-MAJANGA-USALAMA

Mafuriko nchini Afghanistan yaua watu 160

Wizara ya ulinzi imebaini kwamba vikosi vya usalama vya Afghanistan vimekuwa vinasaidia katika shughuli ya uokoaji na kutoa misaada, licha ya kukabiliwa na ghasia zinazotekelezwa na Taliban nchini humo.
Wizara ya ulinzi imebaini kwamba vikosi vya usalama vya Afghanistan vimekuwa vinasaidia katika shughuli ya uokoaji na kutoa misaada, licha ya kukabiliwa na ghasia zinazotekelezwa na Taliban nchini humo. REUTERS

Mafuriko wiki hii nchini Afghanistan yamegharimu maisha ya karibu watu 160 na waokoaji wanaendelea kutafuta watu ambao wamekwama kwenye matope na chini ya vifusi vya nyumba zilizosombwa na maji, mamlaka imesema.

Matangazo ya kibiashara

Mikoa kumi na tatu, hasa kaskazini mwa nchi, imeathirika, kulingana na wizara yenye dhamana ya kukabiliana na majanga.

Katika mkoa wa Parwan peke yake, kaskazini mwa Kabul, watu 116 wamepoteza maisha, zaidi ya 120 wamejeruhiwa na 15 bado hawajulikani waliko, viongozi wamesema.

"Timu za uokoaji zinaendelea na shughuli za uokoaji na zinatafuta miili ya watu waliotoweka," Wahida Shahkar, msemaji wa mkuu wa mkoa wa Parwan amsema.

Wizara ya ulinzi imebaini kwamba vikosi vya usalama vya Afghanistan vimekuwa vinasaidia katika shughuli ya uokoaji na kutoa misaada, licha ya kukabiliwa na ghasia zinazotekelezwa na Taliban nchini humo.

Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, imesema vikosi vyake vikisaidia jeshi la Afghanistan vimepeleka chakula, maji na blanketi kwa maeneo yaliyoathiriwa.