LEBANON-SIASA-USALAMA

Balozi Moustapha Adib ateuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Lebanon

Rais wa Lebanon Michel Aoun wakati wa mkutano na wakuu wa kambi za wabunge, huko Beirut mnamo Mei 6, 2020.
Rais wa Lebanon Michel Aoun wakati wa mkutano na wakuu wa kambi za wabunge, huko Beirut mnamo Mei 6, 2020. DALATI AND NOHRA / AFP

Balozi wa Lebanon nchini Ujerumani, Moustapha Adib, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu nchini Lebanon, baada ya kupata kura nyingi katika kikao cha wabunge kilichoongozwa na rais wa nchi hiyo Michel Aoun, ikulu ya rais nchini Lebanon imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu mteule ameahidi kuunda haraka timu ya 'wataalam' wa mageuzi.

Uteuzi wa Bwana Adib, 48, unakuja saa chache kabla ya kuwasili nchini Lebanon kwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye aliwahimiza viongozi wa Lebanon kuunda haraka "serikali inayowajibika" ambayo itaiondoa nchi hiyo kwenye mgogoro wa kiuchumi na kisiasa.

Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Saad Hariri ilijiuzulu Agosti 10, siku sita baada ya mlipuko ambao uliharibu bandari ya Beirut na sehemu ya mji mkuu wa Lebanon.

Balozi huyo ambaye hafahamiki sana katika ulingo wa kisiasa nchini Lebanon alipendekezwa Jumapili jioni na vigogo wa kisiasa wa madhehebu ya Sunni, akiwemo waziri mkuu wa zamani Saad Hariri.

Viongozi kutoka Magharibi wameitikia wito wa Walebanon wa kutaka mabadiliko makubwa ya kisiasa baada ya mlipuko katika bandari ya Beirut ambao ulisababisha takriban watu 188 kupoteza maisha, na ambapo wanasiasa walitwikwa lawama kwa uzembe na ufisadi.