IRAQ-UFARANSA-USALAMA

Emmanuel Macron ziarani Baghdad kwa mazungumzo na maafisa wa Iraq na Wakurdi

Emmanuel Macron atafanya ziara ya siku moja nchini Iraq baada ya ziara yake nchini Lebanon (hapa, ilikuwa Beirut, Jumanne, Septemba 1, 2020).
Emmanuel Macron atafanya ziara ya siku moja nchini Iraq baada ya ziara yake nchini Lebanon (hapa, ilikuwa Beirut, Jumanne, Septemba 1, 2020). Stephane Lemouton/Pool via REUTERS

Baada ya ziara yake ya siku mbili nchini Lebanon, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaendelea na ziara yake Mashariki ya Kati: leo Jumatano atakuwa nchini Iraq. Ziara ambayo mwanzoni ilitangazwa tu na maafisa wa Iraq kwa sababu za usalama na kisha kuthibitishwa Jumanne jioni na rais wa Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya kwanza ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini Iraq itakuwa ziara ya muhimu. Ni saa chache tu kulingana na maafisa wa Iraqi, muda ambao rais wa Ufaransa anatarajia kufanya katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, bila kuzuru eneo la Erbil katika mkoa unaojitawala nchini humo wa Kurdistan.

Hii ni zaiara ya kipekee na bila shaka ni kwa sababu ya kuzorota kwa hali ya usalama nchini Iraq. Hata hivyo, Emmanuel Macron anaanatarajia kukutana kwa mazungumzo na maafisa wote wa Iraq na Wakurdi.

Masuala yatakayojadiliwa ni mengi kwa sababu Iraq inapitia migogoro mingi kwa sasa: katika sekta ya afya, kama nchi nyingi duniani, lakini pia katika sekta ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Masuala mawili yanaonekana kuwa vipaumbele kwa Ufaransa. Kwanza, suala la tishio la kuepo kwa makundi ya kijihadi. Kundi la Islamic State (IS) limeongeza mashambulizi yake katika miezi ya hivi karibuni na wakati huo huo, Marekani imetangaza kuwa itapunguza wanajeshi wake nchini humo kwa theluthi moja. Kwa hivyo Paris inatafuta kupata usawa wa majeshi ya kigeni katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Suala lingine muhimu ni kuhusu Uturuki, ambayo inaingilia kijeshi kinyume cha sheria Kaskazini mwa Iraq dhidi ya waasi wa Kikurdi wa PKK. Kunaripotiwa una mvutano kati ya Paris na Ankara mashariki mwa Mediterania. Kwa hivyo Emmanuel Macron hawezi kuacha kushughulikia suala hili na maafisa wa Kikurdi.