SAUDI ARABIA-KHASHOGGI-HAKI

Watu wanane wahukumiwa nchini Saudi Arabia kwa mauaji ya Khashoggi

Mwezi Desemba mwaka jana, hukumu tano za kifo zilitolewa katika uamuzi wa awali wa kesi hiyo, na washtakiwa wengine watatu walihukumiwa kifungo cha maisha. Uamuzi uliotolewa leo Jumatatu ni wa mwisho, kimesemakituo cha televisheni cha Al Arabia.
Mwezi Desemba mwaka jana, hukumu tano za kifo zilitolewa katika uamuzi wa awali wa kesi hiyo, na washtakiwa wengine watatu walihukumiwa kifungo cha maisha. Uamuzi uliotolewa leo Jumatatu ni wa mwisho, kimesemakituo cha televisheni cha Al Arabia. REUTERS

Mahakama nchini Saudia imewahukumu leo Jumatatu watu wanane kifungo cha miaka saba hadi ishirini kwa kuhusika katika kifo cha mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, aliyeuawa mwezi Oktoba 2018 katika majengo ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul, kimeripoti kituo cha televisheni Al Arabia.

Matangazo ya kibiashara

Washtakiwa watano wamehukumiwa kifungo cha miaka ishirini gerezani, mwingine amehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani, wawili wa mwisho walmehukumiwa miaka saba, kituo cha televisheni cha umma Ekhbariya kimebaini.

Mwezi Desemba mwaka jana, hukumu tano za kifo zilitolewa katika uamuzi wa awali wa kesi hiyo, na washtakiwa wengine watatu walihukumiwa kifungo cha maisha. Uamuzi uliotolewa leo Jumatatu ni wa mwisho, kimesemakituo cha televisheni cha Al Arabia.

Mei Mosi, familia ya mwandishi wa habari aliyeuawa iliwasamehe wauaji, na hivyo kutengeneza njia ya hukumu nyepesi.

Saudi Arabia haina mfumo wa sheria uliowekwa na, chini ya sheria za Kiislam, msamaha kutoka kwa familia ya mwathiriwa unaweza kuwa msamaha au adhabu.

Baada ya taarifa nyingi zinazokinzana, mamlaka nchini Saudia imekiri kwamba Jamal Khashoggi, ambaye alikuwa amekwenda uhamishoni nchini Marekani, aliuawa na viungo vyake vya mwili kukatwa Oktoba 2, 2018 na maafisa wa Saudi Arabia ambao walitenda uhalifu huo bila kutumwa na yeyote.