UTURUKI-SAUDIA-KHASHOGGI-HAKI

Mauaji ya Khashoggi: Uturuki haikubaliani na uamuzi wa mwisho wa Saudia dhidi ya wauaji

Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi alitoweka baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul Oktoba 2, 2018.
Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi alitoweka baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul Oktoba 2, 2018. Demiroren News Agency / AFP

Uturuki imesema uamuzi wa mwisho wa mahakama ya Riyadh Jumatatu (Septemba 7) kubatilisha hukumu ya kifo iliyotolewa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi huko Istanbul uko 'mbali na ule' ya jamii ya kimataifa ilikuwa inatarajia.

Matangazo ya kibiashara

"Uamuzi wa mwisho ambao mahakama ya Saudia imetoa leo kuhusu mauaji ya kikatili ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa nchi hiyo ya kifalme jijini Istanbul, nchini Uturuki uko mbali na ule ambao Uturuki na jamii ya kimataifa walikuwa wanatarajia," Fahrettin Altun, msemaji wa ikulu ya rais nchini Uturuki ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

Mahakama nchini Saudi Arabia iliondoa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watu watano waliopatikana na hatia ya mauaji ya Jamal Khashoggi, mwaka 2018, vimesema vyombo vya habari.

Waendesha mashitaka walisema kuwa walipewa hukumu ya miaka 20 jela baada ya familia ya Khashoggi ambaye alikuwa ni mwaandishi wa habari kuamua kuwasamehe.

Saudi Arabia haina mfumo wa sheria uliowekwa na, chini ya sheria za Kiislam, msamaha kutoka kwa familia ya mwathiriwa unaweza kuwa msamaha au adhabu.

Kesi hiyo ilipuuziliwa mbali mara tatu na Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Agnes Callamard aliyeitaja kama "isiyofuata sheria " ambaye alisema kuwa Khashoggi alikuwa "muathiriwa wa mauaji ya makusudi, yaliyopangwa " ambayo taifa la Saudi Arabia linawajibika nayo.

Baada ya taarifa nyingi zinazokinzana, mamlaka nchini Saudia imekiri kwamba Jamal Khashoggi, ambaye alikuwa amekwenda uhamishoni nchini Marekani, aliuawa na viungo vyake vya mwili kukatwa Oktoba 2, 2018 na maafisa wa Saudi Arabia ambao walitenda uhalifu huo bila kutumwa na yeyote.