MAREKANI-AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Mike Pompeo kuhudhuria mazungumzo ya amani ya Afghanistan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisaini mkataba wa kihistoria wa amani na kiongozi wa Taliban baada ya miaka 18 ya vita.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisaini mkataba wa kihistoria wa amani na kiongozi wa Taliban baada ya miaka 18 ya vita. KARIM JAAFAR / AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo atahudhuria mazungumzo ya amani kati ya Waafghanistan ambayo yatafunguliwa mwishoni mwa wiki hii huko Doha, Donald Trump ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya nje ya Qatar ilisema jana jioni kwamba viongozi wa Taliban na serikali ya Afghanistan wataanza mazungumzo ya moja kwa moja ya amani Jumamosi. Mazungumzo ambayo pande hizo mbili zimethibitisha.

Hivi karibuni Marekani na Taliban walitia saini kwenye mkataba wa kihistoria ambao unaitaka Marekani kuondoa askari wake nchini Afghanistan.

Mapema wiki hii jeshi la Marekani lilitangaza limefikia hatua ya kupunguza idadi ya wanajeshi wake waliopelekwa nchini Iraq, ambapo idadi ya wanajeshi itashuka kutoka kwa wanajeshi 5,200 hadi 3,000 ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye atawania katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, alifanya kampeni mwaka 2016 akiahidi kukomesha "vita visivyo na mwisho" vya Marekani, ambayo inaendelea kupunguza idadi ya wanajeshi wake katika nchi kama Afghanistan, Iraq na Syria.