ISRAEL-BAHRAIN-UHUSIANO

Israeli na Bahrain zatangaza kuresheja uhusiano wao

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu (kushoto) na Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa al-Khalifa.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu (kushoto) na Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa al-Khalifa. RONEN ZVULUN, Fayez Nureldine / AFP

Israeli na Bahrain zimefikia makubaliano ya kufufua uhusiano wao Ijumaa (Septemba 11), mwezi mmoja baada ya makubaliano kati ya Falme za Kiarabu na nchi hiyo ya Kiyahudi.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo pia lilitolewa, wakati huo huo, na rais wa Marekani Donald Trump, wakati mkataba huo unatarajiwa kutiwa saini rasmi katika Ikulu ya White House wiki ijayo. Bahrain na Israeli sawa na nchi nyingine za Kiarabu katika ukanda huo zimeendelea kuwa na uhasama na Iran.

"Hatua ya kihistoria kuelekea amani katika Mashariki ya Kati", vyanzo kutoka nchini Israeli vimesema. Tangazo la mkataba wa kufufua uhusiano kati ya Israeli na nchi ya Kifalme ya Bahrain lilitolewa wakati mmoja katika Ikulu ya White House na rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

"Huu ni wakati mpya wa amani. Amani badala ya amani. Uchumi badala ya uchumi. Tumewekeza kwa amani kwa miaka mingi. Na sasa ni amani ambayo itawekeza kwetu. Itawezesha uwekezaji mwingi nchini Israeli. Na hii ni muhimu sana, "amesema Benjamin Netanyahu.

Mwezi uliopita, Umoja wa Falme za Kiarabu ulikubali kurejesha uhusiano wa kawaida na Israel chini ya mkataba uliosimamiwa na Marekani unaotarajiwa kutiwa saini katika sherehe itakayoandaliwa katika ikulu ya White House siku ya Jumanne, itakayoongozwa na rais Trump anayetafuta kuchaguliwa tena kama rais katika uchaguzi wa Novemba 3. Sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Falme za Kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed al-Nahyan.