LEBANON-SIASA-USALAMA

Lebanon: Adib anataka ushirikiano kwa kufanikisha mpango wa Macron

Waziri mkuu mteule wa Lebanon, Moustapha Adib, akizungumza mbele ya vyombo vya habari baada ya uteuzi wake, Agosti 31, 2020.
Waziri mkuu mteule wa Lebanon, Moustapha Adib, akizungumza mbele ya vyombo vya habari baada ya uteuzi wake, Agosti 31, 2020. REUTERS/Mohamed Azakir

Waziri Mkuu mteule wa Lebanon ametoa wito kwa vyama vyote vya siasa nchini humo kuwajibika vilivyo katika uundaji wa haraka wa serikali mpya na kufanikisha mpango wa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kujaribu kuiondoa Lebanon kwenye mgogoro unaoendelea.

Matangazo ya kibiashara

"Ucheleweshaji wa uundwaji wa serikali unazidisha mzozo kuwa mbaya zaidi. Lebanon haiwezi kuendelea kupoteza kutokana na mgogoro huu unaendelea kuikumba nchi hii," amesema Mustapha Adib katika taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la serikali.

Ikiwa imesalia wiki moja baada ya muda wa mwisho uliowekwa na Emmanuel Macron, vyama vya siasa nchini Lebanon bado havijafanikiwa kukubaliana juu ya muundo wa serikali mpya, hasa kutokana na Hezbollah na washirika wake kutoka chama cha Kishia cha Amal wanataka wapewe Wizara ya Fedha.