IRAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Rouhani: Marekani inakumbwa na upinzani mkubwa kwa kuiwekea vikwazo Iran

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameishtumu Marekani na kusema kuwa mipango yake imegongwa mwamba, baada ya kukosa uungwaji mkono licha ya vitisho kwa serikali ya Tehran.
Rais wa Iran Hassan Rouhani ameishtumu Marekani na kusema kuwa mipango yake imegongwa mwamba, baada ya kukosa uungwaji mkono licha ya vitisho kwa serikali ya Tehran. Reuters

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani inatengwa na mataifa mengine yenye nguvu, kupuuzia kauli ya Washngton DC kuwa, vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Tehran, vimerejeshewa tena.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Marekani hivi karibuni, ilisema kuwa vikwazo hivyo vilivyokuwa vimesitishwa dhidi ya Iran kufuata mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015, vilikuwa vimerejeshwa na vinatekelezwa kikamilifu.

Kauli ya Washington ilikuja, licha ya kujiondoa kwenye utekelezwaji wa mkataba huo mwaka 2018 unaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi.

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameishtumu Marekani na kusema kuwa mipango yake imegongwa mwamba, baada ya kukosa uungwaji mkono licha ya vitisho kwa serikali ya Tehran.

Vikwazo dhidi ya Iran viliondolewa baada ya Tehran kukubali kuacha kurutubisha madini yake ya uranium, na kuungwa mkono na mataifa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanaoundwa na Ufaransa, China, Urusi, Uingerea pampoja na Ujerumani.

Ujerumani imesema viyisho vya Marekabni havina uzito wowote wa kisheria kuhusu mkataba huo.