LEBANON-USALAMA

Lebanon: Mapigano yazuka kati ya vikosi vya usalama na makundi ya wanamgambo wa Kiislam

Afisa wa vikosi vya usalama vya Lebanon (picha ya kumbukumbu).
Afisa wa vikosi vya usalama vya Lebanon (picha ya kumbukumbu). ANWAR AMRO / AFP

Kumetokea mapigano makali kati ya vikosi vya usalama vya Lebanon na makundi ya wanamgambo wa Kiislam wenye itikadi kali kaskazini mwa Lebanon, karibu na mpaka na Syria, Jumamosi, Septemba 26.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yamesababisha vifo kadhaa katiak kambi ya makundi yenye silaha na wapiganaji wengi kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya salama.

Mapigano hayo yalizuka wakati wa maafisa polisi walikuwa karika operesheni yao katika kijiji kimoja kaskazini mwa Lebanon, ikiwa ni sehemu ya operesheni kubwa ya kuyasaka makundi ya wanamgambo wa Kiislam wanaoshukiwa kupanga mashambulizi.

Watuhumiwa hao, karibu kumi na tano, waliweka upinzani mkali, wakitumia silaha za kivita na mabomu. Vikosi vya usalama vilijibu kwa silaha kubwa kubwa na zile za kurusha mabomo. Milipuko ambayo ilisikika sehemu nyingi kaskazini mwa nchi hiyo.

Septemba 14, wanajeshi wanne waliuawa wakati wa operesheni ya jeshi, Kaskazini mwa Lebanon, nyumbani kwa mwanajihadi, Khaled el-Tellaoui, ambaye alipigwa risasi siku hiyo hiyo. Mshukiwa huyo alihusishwa katika mauaji ya watu watatu, pamoja na maafisa wawili wa polisi wa manispaa, katika kijiji kimoja Kaskazini mwa LIbanon, Agosti 22.