SAUDI ARABIA-G20-USHIRIKIANO

Mkutano wa G20 kufanyika 21 na 22 Novemba Riyadh

Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.
Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia. getty images

Saudi Arabia imetangaza leo Jumatatu kwamba mkutano wa nchi zilizostawi kiviwanda na kiuchumi, G20, utafanyika kwa video tarehe 21 na 22 Novemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la mataifa 20 linakusanya theluthi mbili ya idadi ya watu ulimwenguni, likiwa na asilimia 85 za uchumi na 75 ya biashara.

Mkutano wake wa kilele huwaleta pamoja viongozi kutoka mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea ulimwenguni.

Mkutano huo utakuwa kwa njia ya mtandao badala ya kukutana mjini Riyadh kama ilivyokuwa imepangwa mwanzoni

Katika taarifa yake, Saudi Arabia, imesema mkutano huo utakuwa na kauli mbiu ya "Kuzipa uhalisia fursa za karne ya 21 kwa ajili ya wote".