IRAN-SAUDI ARABIA-USALAMA

Tehran yakanusha kutoa mafunzo kwa kundi la magaidi lililovunjwa na Saudi Arabia

Kulingana na Saudi Arabia, kundi la kigaidilililopewa mapfunzo na vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran limevunjwa mwezi huu wa Septemba na idara za usalama. Watu kumi wamekamatwa pamoja na silaha kadhaa na vilipuzi.
Kulingana na Saudi Arabia, kundi la kigaidilililopewa mapfunzo na vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran limevunjwa mwezi huu wa Septemba na idara za usalama. Watu kumi wamekamatwa pamoja na silaha kadhaa na vilipuzi. Mizan News Agency/WANA Handout via REUTERS

Iran imekanusha madai kwamba kundi la magaidi walioangamizwa na mamlaka nchini Saudi Arabia walipewa mafunzo na vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi nchini humo, runinga ya serikali ya Iran imeripoti.

Matangazo ya kibiashara

"Mashtaka yasiyokoma na yasiyo kuwa ya msingi ya utawala wa Saudia hayatasaidia Riyadh kufikia malengo yake na tunaitaka Saudi Arabia kuchagua njia ya uaminifu na hekima badala ya ile ya matukio ambayo hayana thamani", Saeed Khatibzadeh, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Iran, aliyenukuliwa na televisheni ya serikali amesema.

Kulingana na Saudi Arabia, kundi la kigaidilililopewa mapfunzo na vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran limevunjwa mwezi huu wa Septemba na idara za usalama. Watu kumi wamekamatwa pamoja na silaha kadhaa na vilipuzi.

Msemaji wa ofisi ya rais katika maswala ya amesema kuwa magaidi haowa"walipewa mafunzo ya kijeshi, pamoja na jinsi ya kutengeneza vilipuzi, katika maeneo ya vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran" kwa wiki kadhaa mwishoni mwa mwaka 2017.