LEBANON-SIASA-USALAMA

Wanne wafariki dunia katika mlipuko wa tanki la mafuta Beirut

Watu wanne wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko wa tanki la mafuta lililotokea jana Ijumaa katika jengo moja huko Beirut, limeripoti Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Lebanon.

Mlipuko huo ulisababisha moto mkubwa katika jengo hilo, lililoko katika wilaya ya Tarik al Djadida, kimesema chanzo cha usalama.
Mlipuko huo ulisababisha moto mkubwa katika jengo hilo, lililoko katika wilaya ya Tarik al Djadida, kimesema chanzo cha usalama. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulisababisha moto mkubwa katika jengo hilo, lililoko katika wilaya ya Tarik al Djadida, kimesema chanzo cha usalama.

Mtu mmoja aliyejeruhiwa yuko katika hali mbaya, wengine kadhaa wanatibiwa baada ya kuathiriwa na moshi, Shirika la Msalaba Mwekundu na chanzo kutoka hospitali vimesema.

Hivi karibuni ghala la silaha la Hezbollah liliteketea kwa moto baada ya kutokea mlipuko mkubwa kufuatia "hitilafu ya kiufundi".

Mlipuko wa Agosti 4 katika bandari ya Beirut, ambao uligharimu maisha ya watu karibu 200, umezidi hali ya wasiwasi nchini humo.

Lebanon inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.