AFGHANISTAN-USALAMA

Kumi na nane wauawa katika shambulio la Kabul

Takriban watu 18 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya kituo cha elimu huko Kabul, shamvulio lililotokea siku ya Jumamosi, vyanzo vya usalama kutoka Afghanistan vimebaini.

Wanajeshi wa jeshi la Afghanistan katika eneo la shambulio la kujitoa muhanga huko Kabul mnamo Aprili 29, 2020.
Wanajeshi wa jeshi la Afghanistan katika eneo la shambulio la kujitoa muhanga huko Kabul mnamo Aprili 29, 2020. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani, maiti kumi na tatu zimepatikana na watu 57 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Kulingana na msemaji wa wizara hiyo, mhalifu huyo alilipua vilipuzi katika mtaa ulio karibu na kituo cha elimu cha Denmark.

Kundi la Islamic State, katika taarifa, limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Msemaji wa Taliban amekanusha kuhusika kwa shambulio hilo.