PAKISTANI-USALAMA

Saba wauawa na 50 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu Pakistan

dadi ya waliofariki imeongezeka hadi 7 na 50 kujeruhiwa, Mohammad Ali Gandapur, afisa mwingine, ameliambia shirika la habari la AFP.
dadi ya waliofariki imeongezeka hadi 7 na 50 kujeruhiwa, Mohammad Ali Gandapur, afisa mwingine, ameliambia shirika la habari la AFP. AFP

Takriban watu saba wameuawa na 50 wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu leo Jumanne katika cho cha kidini (madrasat) huko Peshawar, jiji kubwa la Kaskazini Magharibi mwa Pakistan, vyanzo vya polisi vimesema.

Matangazo ya kibiashara

"Mlipuko huo ulitokea wakati visomo vya Qor'an vimekuwa vikitolewa. Mshambuliaji aliingia na mkoba (uliokuwa na bomu) ndani ya chuo hicho cha kidini," Waqar Azim, afisa wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP.

Mtu huyo aliyoingiza mkoba huo uliokuwa umetegwa bomu aliondoka eneo la tukio muda mfupi kabla ya mlipuko huo, Waqar Azim ameongeza.

Visomo hivyo vilikuwa vinarushwa moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook. Video hiyo inaonyesha kiongozi wa kidini, akivaa mavazi meupe na kilemba kichwani, akisoma Aya za Qor'an na kutafsiri kwa lugha ya Pashtun na Kiarabu mbele ya kipaza sauti, kabla ya mlipuko huo kumkatiza, huku kelele nyingi zikisikika.

Idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 7 na 50 kujeruhiwa, Mohammad Ali Gandapur, afisa mwingine, ameliambia shirika la habari la AFP. Ripoti ya awali iliripoti watu 4 waliuawa na 34 walijeruhiwa.

Kulingana na Mohammad Asim Khan, msemaji wa hospitali ya eneo hilo, miili saba na watu 70 waliojeruhiwa wamepelekwa katika kituo chake.

Wote waliofariki dunia walikuwa watu wazima wenye umri kati ya miaka 20 na 40, wakati wengine waliojeruhiwa walikuwa watoto, aliongeza.

Katika chuo hicho, kulikuwa na sehemu mbili, moja ya watu wazima na moja ya watoto, alisema Safiullah Khan, mmoja wa walimu. Mlipuko huo mkubwa, uliosikika katika vitongoji vingi vya Peshawar, ulitokea "katika sehemu ambayo wanasomea wanafunzi wenye umri wa zaidi ya miaka 18", amebaini, akiongeza kuwa watu wengi ikiwa ni pamoja na watu kadhaa walijeruhiwa kufuatia kuanguka kwa ukuta baada ay mlipuko huo.