IRAQ-USALAMA

Iraq: Kumi na moja waangamia katika shambulizi dhidi ya kituo cha jeshi

Watu wasiojulikana waliojihami kwa silaha wameendesha shambulio dhidi ya kituo cha jeshi la Iraq magharibi mwa mji mkuu Baghdad, na kusababisha vifo vya watu 11na 8 kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na askari mmoja, polisi na vyanzo vya hospitali vimesema leo Jumatatu.

Operesheni ya pamoja ya jeshi na polisi imeanza ili kuwasaka wahusika wa shambulio hilo, vyanzo vya polisi vimebaini.
Operesheni ya pamoja ya jeshi na polisi imeanza ili kuwasaka wahusika wa shambulio hilo, vyanzo vya polisi vimebaini. REUTERS/Alaa Al-Marjani
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji walikuwa kwenye magari manne na walikuwa wamejihami kwa mabomu na bunduki za kivita, vyanzo hivyo vimeongeza.

Operesheni ya pamoja ya jeshi na polisi imeanza ili kuwasaka wahusika wa shambulio hilo, vyanzo vya polisi vimebaini.

Hata hivyo hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Iraq inaendelea kushuhudia visa vya mauaji na mdororo wa usalama katika maeneo mbalimbali.