MAREKANI-IRAN-USHIRIKIANO

Marekani kuichukulia vikwazo Iran kutokana na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji

Marekani inatarajia kuchukuwa vikwazo wiki ijayo dhidi ya maafisa wa Irani kwa kuhusika kwao katika ukandamizaji mkali wa maandamano ya mwaka jana dhidi ya serikali nchini Iran, vyanzo vitatu rasmi vimebaini.

Rais wa Iran Hassan Rouhani wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Tehran, Februari 16, 2020.
Rais wa Iran Hassan Rouhani wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Tehran, Februari 16, 2020. Official Presidential website/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na moja ya vyanzo hivyo, vikwazo hivyo, vinalenga watu kadhaa na kambuni kadhaa za Irani.

"Ikiwa hii itathibitishwa, itaonyesha tu kutapa tapa kwa utawala ambao uadui wao kwa watu wa Irani unajulikana," Alireza Miryousefi, msemaji wa ujumbe wa Irani kwa Umoja wa Mataifa huko New York amesema katika taarifa.

Karibu watu 1,500 waliuawa katika kipindi kisichozidi wiki mbili baada ya maandamano kuanza mnamo Novemba 15, 2019, kulingana na shirika la habari la REUTERS, ikinukuu maafisa watatu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran.