PAKISTANI-USALAMA

Katuni za Muhammad: Waandamanaji waombwa kusitisha maamndamano Pakistan

Makabiliano yalizuka siku moja kabla kati ya wafuasi wa vuguvugu hilo na polisi huko Islamabad wakati wa moja ya maandamano haya.
Makabiliano yalizuka siku moja kabla kati ya wafuasi wa vuguvugu hilo na polisi huko Islamabad wakati wa moja ya maandamano haya. REUTERS

Vuguvugu la Kiislamu nchini Pakistan la Tehrik-i-Labaik limetoa wito wa kusitishwa kwa maandamano dhidi ya kuchapishwa katuni za Muhammad nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati serikali ya nchi hiyo iliwataka wananchi wake kususia bidhaa kutoka Ufaransa.

Makabiliano yalizuka siku moja kabla kati ya wafuasi wa vuguvugu hilo na polisi huko Islamabad wakati wa moja ya maandamano haya.

"Tumeamua kusitisha maandamano yetu baada ya serikali kutia saini makubaliano ambayo imesema itaidhinisha rasmi kususiwa kwa bidhaa za Ufaransa," msemaji wa vuguvugu la Tehrik-i-Labaik Ejaz Ashrafi amesema kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Gazeti la kila wiki la Charlie Hebdo lilichapisha tena katuni za Muhammad mwezi wa Septemba mwaka huu wakati wa kufunguliwa kwa kesi ya shambulio ambalo lilisababisha vifo vya watu kumi na wawili kwenye majengo yake mnamo mwezi Januari 2015, baada ya chapisho la kwanza.