SYRIA-ISRAEL-USALAMA

Kumi waangamia katika mashambulizi ya Israel Syria

Angalau wapiganaji kumi, wakiwemo maafisa watatu wa jeshi la ulinzi wa anga la Syria na wanamgambo wa kigeni, wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na jeshi la Israeli Jumatano hii (Novemba 18) nchini Syria, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria la OSDH.

jeshi la Israel mapema Jumatano asubuhi limethibitisha kwamba lilitekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya  ngome za wanamgambo wa Iran na jeshi la Syria kwa kulipiza kisasi baada ya kugundua vilipuzi kando ya mpaka wa kaskazini wa taifa hilo la Kiyahudi.
jeshi la Israel mapema Jumatano asubuhi limethibitisha kwamba lilitekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za wanamgambo wa Iran na jeshi la Syria kwa kulipiza kisasi baada ya kugundua vilipuzi kando ya mpaka wa kaskazini wa taifa hilo la Kiyahudi. IAF handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo watano "wanaodaiwa kuwa na uraia wa Irani, ambao ni wa Kikosi cha Quds", lakini pia wapiganaji wawili wa wanamgambo wanaounga mkono Iran, ni miongoni mwa watu hao kumi waliouawa, OSDH imebaini.

Wakati huo huo jeshi la Israel mapema Jumatano asubuhi limethibitisha kwamba lilitekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za wanamgambo wa Iran na jeshi la Syria kwa kulipiza kisasi baada ya kugundua vilipuzi kando ya mpaka wa kaskazini wa taifa hilo la Kiyahudi.

"Kilichofanywa na Iran na Syria: Waliweka vifaa vya kulipuka karibu na eneo la Alfa ili kuwalipua wanajeshi wa Israeli. Tulichofanya: tmeendesha mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za kikosi cha Quds cha Irani na kikosi cha wanajeshi cwa Syria nchini Syria, ”jeshi la Israeli limeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.