MAREKANI-AFGHANISTAN-USALAMA

Marekani kupunguza wanajeshi wake Afghanistan na Iraq ifikapo Januari 2021

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Christopher Miller, akiwa Pentagon mnamo Novemba 13, 2020.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Christopher Miller, akiwa Pentagon mnamo Novemba 13, 2020. AP Photo/Manuel Balce Ceneta

Marekani inatarajia kupunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Afghanistan hadi 2,500 mnamo mwezi Januari 2021, kikosi kidogo kabisa cha nchi hiyo katika miongo miwili ya vita, na wanajeshi wengine 500 wataondoka nchini Iraq makao makuu ya jeshi Marekani imesema.

Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi tu baada ya tangazo hilo, roketi zlurushwa kwenye ubalozi wa Marekani nchini Afghanistan.

Karibu wanajeshi 2,000 wataondolewa nchini Afghanistan ifikapo Januari 15, na wengine 500 wataondoka Iraq na watabaki wanajeshi 2,500 tu kwa kila nchi, kaimu waziri mpya wa ulinzi Christopher Miller amesema.

Zoezi hilo la kundoa wanajeshi hao katika nchi hizo mbili litafanyika wakati Donald Trump, aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais na Joe Biden kutoka chama cha Democratic kuibuka mshindi, atakabidhi madaraka mnamo Januari 20.

Wakati huo huo Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, imeonya dhidi ya Marekani kuondowa wanajeshi wake Afghanistan.

Mkuu wa Shirika la Kujihami la NATO, Jens Stoltenberg, ameonya kwamba hatua ya Marekani kuondowa kwa ghafla wanajeshi wake nchini Afghanistan kunaweza kuigeuza nchi hiyo kuwa "jukwaa la magaidi wa kimataifa."