SAUDI ARABIA-G20-CORONA-USHIRIKIANO

Suala la ugonjwa wa COVID-19 kugubika mkutano wa G20 Saudi Arabia

Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, huko Diriya (Saudi Arabia), Desemba 7, 2019
Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, huko Diriya (Saudi Arabia), Desemba 7, 2019 Saudi Royal Palace/AFP/Archives Texte par : RFI Suivre

Mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yaliyostawi na yale yanayoinukia kiuchumi, G20, unaanza leo Jumamosia nchini Saudi Arabia, mkutano ambao utagubikwa na suala la ugonjwa wa COVID-19.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo pia watazungumzi kuhusu misaada ambayo nchi tajiri zinaweza kutoa au la kwa nchi masikini zilizoathirika na mgogogo wa kiuchumi na mzigo mkuwa wa madeni.

Tuna imani kutoka kwa mkutano huu wa G20 uratibu bora wa mipango kuinua bajeti. Dola Trilioni 12 zimetumika kukabiliana na mgogoro huu wa kiafya duniani. Lakini bado kuna ukosefu wa mkakati wa nchi nyingi kuondokana na mgogoro huo. Kuhusu suala hili, Umoja wa Ulaya unatarajia mengi kutoka kwa utawala mpya wa Marekani.

Shirika la Fedha la Kimataifa pia limezitaka nchi za G20 "kuondoa" vizuizi vya kibiashara vilivyowekwa "katika miaka ya hivi karibuni" kuuunga mkono kurejea kwa shughuli za kawaida na kuzuia kuanguka kwa uchumi wa dunia, kkulingana na kauli ya Katibu Mkuu aw Uomoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Kulingana na rasimu ya taarifa ya pamoja itakayotolewa na viongozi watakaohudhuria, kundi la G20 litaahidi kufanya kila linalowezekana kudhibiti kusambaa janga la virusi vya corona huku likitahadharisha kuwa ufufuaji wa uchumi wa dunia bado unakabiliwa na ukosefu wa usawa na mazingira yasiyotabirika.

Viongozi wa kundi hilo wametanabaisha kuwa mzozo wa virusi vya Corona umeziathiri zaidi jamii masikini na kusema mataifa anayoendelea yatahitaji msaada zaidi wa kupunguziwa mzigo wa madeni hata baada ya kipindi cha sasa cha hadi mwishoni mwa mwezi Juni, 2021.

Hata hivyo shinikizo limetolewa la kutaka kundi la mataifa ya G20 kufidia nakisi ya dola bilioni 4.5 iliyopo kwenye mpango wa kusambaza chanjo ya virusi vya corona wa shirika la afya duniani WHO na kufungua njia ya kumalizika kwa janga hilo.