SYRIA-IRAN

Afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Iran auawa kwenye mpaka wa Syria na Iraq

Wanajeshi wa Israel, wakifanya doria kwenye mji wa Rafah, ukanda wa Gaza.
Wanajeshi wa Israel, wakifanya doria kwenye mji wa Rafah, ukanda wa Gaza. REUTERS/Micha Han/GPO

Maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Iran wanaendelea kulengwa na mashambulizi ya kuvizia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na nchi jirani.

Matangazo ya kibiashara

Siku chache baada ya mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi aliyeanzisha programu ya nyuklia ya taifa hilo miongo miwili iliyopita, afisa mwengine wa jeshi la Iran aliuawa Jumamosi wiki iliyopita.

 

Kamanda huyo wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran aliuawa mwishoni mwa wiki iliyopita katika shambulio la anga kwenye mpaka wa Iraq na Syria, maafisa wa usalama wa Iraq na vyanzo kutoka kundi la wanamgambo nchini humo wamebaini.

 

Jina la kamanda huyu wa Pasdaran halijatangazwa. Kamanda huyo aliuawa ndani ya gari lake akiwa pamoja na watu wengine watatu, vyanzo hivyo vimeongeza.

 

Gari hilo, ambalo lilikuwa limebeba silaha kwenda nchini Syria, lilishambuliwa baada ya kuvuka mpaka, vyanzo viwili kutoka idara ya usalama nchini Iraq vimesema.

 

Shambulio hilo la anga lilitokea Jumamosi au Jumapili, vyanzo hivyo vimeongeza, bila hata hivyo kutaka kutaja tarehe halisi.