AFGHANISTAN

Naibu Gavana wa Kabul auawa katika shambulio la kigaidi

Afisa usalama wa Afghanistan, akipita katika moja ya eneo ambalo lilishambuliwa hivi karibuni
Afisa usalama wa Afghanistan, akipita katika moja ya eneo ambalo lilishambuliwa hivi karibuni REUTERS/Omar Sobhani

Shambulio la bomu limegharimu maisha naibu gavana wa mji wa Kabul leo Jumanee, kulingana na idara za usalama nchini Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

Bomu lilikuwa limewekwa chini ya gari la Mahboobullah Mohebi, naibu gavana wa mji wa Kabul, kulingana na vyanzo hivyo.Walinzi wawili wamejeruhiwa. Hakuna kundi lolote kufikia sasa limedai kuhusika na shambulio hilo.

 

Serikali ya Afghanistan na Taliban walianza mazungumzo ya amani chini ya mwavuli wa Marekani mwezi Septemba, lakini wanamgambo wa Kiislam hawajasalimisha silaha zao na mashambulizi yanashuhudiwa mara kwa mara, haswa katika mji mkuu, ambapo mwendesha mashtaka aliuawa wiki iliyopita.

 

Maelfu ya watu wameuawa nchini Afghanistan katika mashambulizi mbalimbali ya makundi yenye silaha, huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiendelea kuonyooshea kidole cha lawama kundi la Taliban na washirika wake.