SYRIA-ISRAEL

Syria: Shambulizi la anga la Israel laua mtu mmoja Damascus

Jeshi la Syria katika mkoa wa Allepo
Jeshi la Syria katika mkoa wa Allepo AFP

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Syria imezuia "chokochoko za Israeli" katika anga ya mji mkuu wa Dameski, shirika la habari la serikali la Sana limeripoti leo Jumatano asubuhi, likinukuu mmoja wa waandishi wake.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili limesababisha kifo cha mtu mmoja nje kidogo ya mji wa Damascus wakati wanajeshi watatu wamejeruhiwa, kulingana na chanzo cha jeshi kilichonukuliwa na shirika la habari la serikali ya Syria.

Jeshi la Syria halijatoa maelezo yoyote kuhusiana na shambulio hilo.

Israeli, ambayo inaona Iran kama tishio lake kuu katika eneo hilo, imekuwa ikitekeleza mara kwa mara mashambulizi nchini Syria dhidi ya ya maslahi ya Iran na wanamgambo wanaounga mkono Irani, kama vile Hezbollah kutoka Lebanon, kundi linalosaidia utawala wa rais wa Syria Bashar al Assad.