SAUDI ARABIA-QATAR

Saudi Arabia yafungua mipaka na nchi ya Qatar

Barabara ya Saudi Arabia
Barabara ya Saudi Arabia Reuters

Saudi Arabia imetangaza kufungua tena viwanja vyake vya ndege kwa ndege kutoka Qatara pamoja na mipaka na nchi hiyo,  baada ya zaidi ya miaka mitatu ya kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili za Ghuba.

Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo ilitangazwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Kuwaiti.

"Kulingana na pendekezo kutoka kwa Emir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah, ilikubaliwa kufungua viwanja vya ndege na vile vile mipaka ya ardhini na baharini kati ya Saudi Arabia na Qatar kuanzia  Jumatatu jioni, ametangaza Sheikh Ahmed Nasser Al-Sabah katika taarifa ya televisheni, bila kutoa maelezo zaidi.

Tangazo hilo linakuja usiku wa kuamkia mkutano unaotarajiwa sana wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) nchini Saudi Arabia, wakati ambapo Riyadh na pia nchi zingine - ikiwa ni pamoja na na Qatar zinatarajia kuboresha maridhiano.

Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri zilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Qatar mwezi Juni 2017, zikiituhumu kuwa inaunga mkono wanamgambo wa Kiislamu, kuwa na uhusiano na Iran na kusababisha vurugu katika kanda hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Kuwait ameongeza kuwa Emir wa Kuwait, ambaye hufanya kazi kama mpatanishi katika mzozo wa Ghuba, alizungumza kwa njia ya simu na viongozi wa Saudi arabia na Qatar. Watatu hao walitoa wito kwa 'umoja' wa nchi za Ghuba kwenye mkutano huo wa Jumanne, amesema.

Emir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani, amealikwa rasmi kwenye mkutano huo kama miaka ya nyuma, lakini hakuwahi kuhudhuria. Lakini muda mfupi baada ya tangazo la waziri wa Kuwait, taarifa kutoka ofisi ya Qatar Emir ilitangaza kwamba atashiriki mkutano huo.

"Emir atashiriki katika mkutano wa GCC utakaofanyika Jumanne katika mkoa wa Al-Ula katika nchi jirani ya Saudi Arabia," imesema taarifa hiyo.

Marekani ambayo ilikuwa ikitaka kuunganisha nchi za Kiarabu dhidi ya Iran, imetoa shinikizo kwa kuzipatanisha nchi hizi za Ghuba zilizokuwa katika uhasama kwa miaka mingi, ambazo zote ni washirika wa kimkakati wa Washington.