Papa Francis asita kuzuru Iraq mwezi Machi kwa sababu ya COVID-19
Imechapishwa:
Kiongozi wa kanisa Katolika duniani Papa Francis hana uhakika wa kuzuru nchi ya Iraq kutokana na ongezeko la visa vya maambukizi linaloripoitwa nchini humo kaika siku za hivi karibuni, kulingana na vyanzo kutoka Vatican.
Safari ya kitume iliyopangwa mwezi Machi nchini Iraq inaweza isifanyike kwa sababu ya mgogoro wa kiafya, Papa Francis amesema siku ya Jumapili.
"Ndio, imebidi nisitishe safari kwenda nchini Iraq, kwa sababu sikutaka nisababishe mikusanyiko mikubwa. Maisha yamebadilika," amesema katika mahojiano na kituo cha Runinga cha Kanale 5 cha Italia.
Ziara hiyo ya kwanza ya Papa nchini Iraq, iliyopangwa kuanzia Machi 5 hadi 8, ingelimfikisha kiongozi huyo katika mji mkuu Baghdad, lakini pia katika mji wa Uru, mji uliotajwa katika Agano la Kale, lakini pia katika miji ya Erbil, Mosul na Bakhdida, katika eneo la Ninawi.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 84 anatarajiwa kupewa chanjo wiki hii dhidi ya COVID-19.