YEMEN-MAREKANI

Yemen: Marekani yataja waasi wa Houthi kama kundi la kigaidi

Waasi wa Houthi nchini Yemen
Waasi wa Houthi nchini Yemen REUTERS/Khaled Abdullah

Serikali ya Marekani ya Donald Trump imetangaza kwamba italiweka kundi la waasi wa Houthi nchini Yemen kwenye orodha yake ya makundi ya kigaidi, siku kumi kabla ya kumalizika kwa muhula wa rais huyo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashirika ya kimataifa hatua hiyo ya utawala wa Trump inaweza kuhatarisha hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi.

Vikwazo hivi vinalenga kuwahusisha waasi wa Houthi katika vitendo vyao vya kigaidi, hasa kwa mashambulio yao wanapovuka mipaka ya nchi jirani na kutishia raia usalama wao, miundombinu na usafirishaji wa bidhaa baharini," Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema katika taarifa iliyotolewa Jumapili usiku.

Waasi wa Houthi wameendelea kutekeleza mashambulizi katika maeneo ya mipakani ya Saudi Arabia, nchi inayoongoza muungano wa Kiarabu unaopambana na waasi hao.